africa.lawBeta
SearchAsk AICollectionsJudgesCompareMemo
africa.law

Free access to African legal information. Legislation, case law, and regulatory documents from across the continent.

Resources

  • Legislation
  • Gazettes
  • Jurisdictions

Developers

  • API Documentation
  • Bulk Downloads
  • Data Sources
  • GitHub

Company

  • About
  • Contact
  • Terms of Use
  • Privacy Policy

Jurisdictions

  • All jurisdictions →

© 2026 africa.law by Bhala. Open legal information for Africa.

Aggregating legal information from official government publications and public legal databases across the continent.

Back to search
Case Law[2026] TZHC 2917Tanzania

Mtungwa Nasibu vs Monika Juma (Maombi No. 9533 of 2026) [2026] TZHC 2917 (4 Juni 2026)

High Court of Tanzania

Judgment

MAHAKAMA YA TANZANIA MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MASJALA NDOGO KIGOMA INAYOKETI KIGOMA MAOMBI NO. 000009533 OF 2026 MTUNGWA NASIBU .............................. MLALAMIKAJI/ MRUFANI/ MWOMBAJI/ MDAI DHIDI YA MONIKA JUMA .............................. MJIBU MAOMBI/ MRUFANIWA/ MDAIWA UAMUZI RWIZILE, J Mleta maombi, anaomba kuongezewa muda wa kukata rufaa nje muda. Maombi haya kama ilivyoada yameambatana na kiapo cha mleta mombi. Kiapo chake hata hivyo kimepingwa kwa kiapo kinzani cha mjibu maombi. Wahusika, hawana uwakilishi, hivyo wameeleza maombi haya kwa kifupi mbele yangu. Kurasa. 1

Kumbukumbu zinaonyesha, Mleta maombi alishindwa katika Mgogoro wa Ardhi kati yake na Mjibu maombi. Ilikuwa katika Maombi ya Ardhi Namba 01 ya 2023. Katika Maombi hayo, yaliyotolewa uamuzi tarehe 13.10.2025, Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya Kigoma lilimpatia ushindi Mjibu Maombi. Hivyo alitamkwa kuwa mmiliki wa eneo la mgogoro. Hata hivyo, Mleta Maombi alikata rufaa katika Mahakama haya, rufaa Namba 29218 ya mwaka 2025. Rufaa hiyo ambayo ilisajiliwa kwa wakati yaani tarehe 19.11.2025, ilifutwa kwa sababu ya makosa katika majina yake (Mtungwa Nasibu Mtungwa) ambayo hayasomeki katika Maombi Namba 01 ya 2023, yanayosomeka Mtungwa Nasibu. Baada ya rufaa yake kutupwa mnapo tarehe 11. 03. 2026, hata hivyo alileta maombi haya akiomba apewe tena fursa ya kuleta rufaa yake. Kama nilivyoonesha hapo awali, wahusika hawana uwaskilishi hivyo walisimama wenyewe. Mjibu Maombi katika kupinga alisema hakuna sabubu za msingi za kuruhusu maombi haya kwani Mleta Maombi hukuwa kifungoni au kuwa nje ya nchi. Hivyo ni maoni yake, kilicho sababisha kuchelewa ni uzembe wake tu. Katika kiapo na ufafanuzi wake mleta maombi anaamini tatitzo sio la kwake bali ni mahakama kwani ndiyo walimsaidia kusajili rufaa yake kwa kutumia kitambulisho cha NIDA chenye majina tofauti na yalisomeka katika hukumu ya Baraza Kurasa. 2

Baada ya kupitia kumbukumbu za rufaa yake iliyofutwa na mahakama haya, nimeona hoja yake inamashiko. Kwani nakala ngumu ilisajiliwa ilikuwa na majina sahihi kama yanavyosomeka katika shauri na kumbukumbu za Baraza. Hivyo kama mahakama ingezitia hili, angepwa fursa ya kufanya marekebisho katika mfumo kitu ambacho kinaruhusiwa kisheria. Lakini pia Kanuni za ufunguaji wa mashauri katika mtandao zinatoa mwanya huo. Nimetafari hoja za pande zote mbili. Nimeridhika kwamba pamoja na kwamba baada ya rufaa yake kufutwa, tarehe 11. 03. 2026, alichukua taribani siku 37 kufungua maombi haya yaani tarehe 17.04. 2026. Ninaamini kwa mazingira ya shauri hili, muda aliochelewa unavumilika. Kwa hiyo, Mahakama inaona makosa yaliyofanyika hayakuwa ya kwake. Hivyo Maombi haya yanakubaliwa. Mjibu Maombi anapewa Muda was siku 21 kuanzia leo kuleta rufaa yake, yaani kabla au ifikapo tarehe 24.06.2026. Kila upande utajilipia gharama zake. Imetolewa katika AKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MASJALA NDOGO KIGOMA INAYOKETI KIGOMA tarehe 4 Juni 2026. A. K RWIZILE JAJI Kurasa. 3

Discussion