Idris Community Registered Trustees & Others vs Sheikh Magoso Ahmed & Others (Maombi ya Madai Na. 2594 ya 2025) [2026] TZCA 440 (27 April 2026)
Judgment
KATIKA MAHAKAMA YA RUFANI YA TANZANIA DODOMA MAOMBI YA MADAI NA. 2594 YA 2025 BAINA YA IDRIS COMMUNITY REGISTERED TRUSTEES TARIKA ASKARIA SHADHIRIA....................................MLETA MAOMBI WA 1 SHEIKH SALIM IDRISSA SAAD . .................................. MLETA MAOMBI WA 2 USTAADH ABDULMALICK HEMED HASHIL . .................................................... .... MLETA M USTAADH IDRISSA JUMA KAWAMBWA ...................... MLETA MAOMBI WA 4 USTAADH IDRISSA JUMA ISSA .................... . ........... MLETA MAOMBI WA 5 USTAADH ABDULMAJID ABBAS ABDALLAH ............ ....MLETA MAOMBI WA 6 RAJABU MASHAKA MATIKU............................ . ........ MLETA MAOMBI WA 7 MUDR RAMADHANI ABDALLAH KALENGO .................. MLETA MAOMBI WA 8 USTAADH SAAD OMAR IDRISSA ................... . ..... .....MLETA MAOMBI WA 9 BINT FATUMA RUBEA KARAMA ............................... MLETA MAOMBI WA 10 DHIDI YA SHEIKH MAGOSO A H M ED .................. . ........................ MJIBU MAOMBI WA 1 KABIDHI WASH MKUU WA SERIKALI ..........................MJIBU MAOMBI WA 2 MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI...........................MJIBU MAOMBI WA 3 (Maombi ya kusimamisha utekelezaji wa Uamuzi na Amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam) fMbaqwa, J .^ t ya tarehe 7 Novemba, 2025 katika Maombi va Madai Na. 8896 va 2025 UAMUZI 17 & 27 Aprili, 2026 GALE BA, J.R.: Maombi haya ni ya kusitisha kwa muda utekelezaji wa amri iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es i
Salaam, iliyoketi Dar es Salaam (yaani Mahakama Kuu). Ni rai ya waombaji katika maombi haya, kwamba utekelezaji wa amri iliyotolewa katika Maombi ya Madai Na. 8896 ya mwaka 2025 mbele ya Mheshimiwa Jaji Mbagwa wa Mahakama Kuu, usimamishwe kwa muda ili kusubiria usikilizwaji na hukumu ya Mahakama hii katika Rufaa ya Madai Na. 2430 ya 2025 iliyokwisha wasilishwa mahakamani hapa na waleta maombi. Katika amri inayolengwa na maombi haya ili isimamishwe utekelezaji wake, muombaji wa pili hadi wa kumi walitangazwa kuwa siyo wadhamini halali wa mwombaji wa kwanza, na wakaamriwa kurejesha mali za mwombaji huyo wa kwanza kwa wadhamini wa awali waiiokuwa wamechaguliwa tarehe 23 Februari 2014, hadi pale wadhamini wapya watakapochaguliwa, kwa mujibu wa sheria. Amri hiyo ilitolewa mnamo tarehe 7 Novemba, 2025. Kufuatia uamuzi huo, mnamo tarehe 28 Novemba, 2025, mjibu maombi wa kwanza aliwasilisha Maombi Na. 31136 ya 2025 (maombi ya kutekeleza amri ya Mahakama) katika Mahakama Kuu akiiomba mahakama hiyo iamuru waleta maombi wakabidhi kwake majengo matatu yafuatayo: kwanza, jengo la Msikiti Idrissa lililojengwa kwenye Kiwanja Na. 25, Kitalu "H", Mitaa ya Bonde/Tandamti/Likoma, eneo ia Kariakoo, Dar es Salaam; pili, jengo lililojengwa kwenye Kiwanja Na. 67, Kitalu "G", Mtaa wa Tandamti, eneo la Kariakoo, Dar es Salaam; na tatu, Jengo
kwenye Kiwanja Na. 69, Kitalu "G", Mtaa wa Tandamti, eneo la Kariakoo, Dar es Salaam. Waombaji walipata taarifa za uwepo wa maombi ya kutekeleza amri ya Mahakama mnamo tarehe 17 Desemba, 2025. Tarehe 29 Desemba, 2025, waombaji waliwasilisha maombi haya Mahakamani hapa wakiiomba Mahakama hii itoe amri ya kusitisha kwa muda utekelezaji wa amri ya Mahakama Kuu hadi pale rufaa yao niliyoitaja hapo juu itakaposikilizwa na kuamuliwa. Mbele yangu katika maombi haya, waombaji waliwakilishwa na Wakili Msomi Bwana Buruhani Mussa, wakati mjibu maombi wa kwanza akiwakilishwa na Mawakili Wasomi Bwana Juma Nassoro na Bwana Daimu Halfani. Mjibu maombi wa pili na wa tatu waliwakilishwa na Wakili wa Seri kali Mwandamizi Msomi, Bwana Swalehe Njoma. Katika kuunga mkono maombi haya, Wakili Msomi Bwana Mussa alieleza kwamba maombi yamekidhi masharti yote ya msingi kama yalivyowekwa chini ya Kanuni ya 11 (4), (5) na (7) za Kanuni za Mahakama ya Rufani ya Tanzania za 2009 (Kanuni za Mahakama hii). Kuhusu uzingatiaji wa Kanuni ya 11 (5) (a) ya Kanuni za Mahakama hii, Bwana Mussa aliwasilisha kwamba yaliyoelezwa kwenye aya ya 8 ya kiapo chake yanaonesha dhahiri kwamba endapo maombi haya 3
hayatakubaliwa na utekelezaji wa amri ya Mahakama Kuu ukaachwa uendeiee, basi wateja wake watapata hasara kubwa. Akielezea namna ambavyo wateja wake wataathirika kwa kupata hasara kubwa, Wakili Msomi Bwana Mussa alisema; kwanza, kwa sasa waombaji ndio wanaosimamia uendeshaji wa miradi ya mleta maombi wa kwanza na wanafanya vizuri sana katika kutekeleza jukumu hilo; na pili, kwamba mjibu maombi wa kwanza ana historia mbaya ya kushindwa kutoa taarifa sahihi za fedha za mwombaji wa kwanza. Hi kuthibitisha hoja hii ya pili, Bwana Mussa alieleza kwamba tangu mjibu maombi wa kwanza alipochaguliwa mwaka 2014 hadi mwaka 2019 alipomaliza muda wake wa uongozi, hakuwahi kuwasilisha kwa wadhamini wenzake taarifa yoyote ya fedha za mwombaji wa kwanza. Kutokana na sababu hizo mbili, wakili Mussa akaeleza kwamba ni dhahiri kabisa kwamba, kama maombi haya yatakataliwa, waombaji wataathirika vibaya sana kwa kupata hasara kubwa, kama inavyotamkwa katika Kanuni ya 11 (5) (a) ya Kanuni za Mahakama hii. Kwa hiyo wakili msomi akaomba amri ya kusitisha utekelezaji kusubiria kusikilizwa kwa rufaa itofewe kama ilivyoombwa. Kujibu hoja za Bwana Mussa, alikuwa ni Bwana Nassoro ambaye pakubwa alikubaliana na wakili mwenzake Bwana Mussa, kwamba waombaji walikuwa wamekidhi masharti yaliyo mengi chini ya Kanuni ya
11 ya Kanuni za Mahakama hii, isipokuwa hawakutekefeza matakwa ya kanuni ndogo ya (5) (a) ya Kanuni ya 11 ya Kanuni za Mahakama hii. Alieleza kwamba hakuna hoja za kuridhisha katika kiapo cha Bwana Mussa zinazoonesha kuwa waombaji watapata hasara kubwa iwapo maombi ya kutekeleza amri ya Mahakama hayatasitishwa. Aliendelea kuwasilisha kwamba hoja zilizotolewa na Bwana Mussa wakati wa usikilizwaji mbele ya Mahakama hii, ni hoja zake binafsi zilizotolewa kutoka kwake kama wakili, bila kuwa na uhusiano wowote na kumbukumbu katika jalada la maombi haya. Jambo hilo, wakili Nassoro alidai kuwa ni kinyume na utaratibu wa taaiuma ya uwakili. Kwa ujumla, aliiomba Mahakama itupilie mbali maombi haya kwa kushindwa kukidhi matakwa ya Kanuni ya 11 (5) (a) ya Kanuni za Mahakama hii. Kwa upande wake, Wakili wa Serikali Mwandamizi Bwana Njoma aliunga mkono maombi hayo na kuongeza hoja moja zaidi. Alidai kwamba utekelezaji wa amri ya Mahakama Kuu unapaswa kusitishwa kwa sababu ili mjibu maombi wa kwanza aweze kuchukua uongozi wa mwombaji wa kwanza, sharti athibitishwe kwanza na mjibu maombi wa pili kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo, Sura ya 108 ya Sheria za Nchi. Alisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria tajwa, mjibu maombi wa pili haruhusiwi kutoa idhini kwa mjibu maombi wa kwanza kushika mamlaka katika ofisi ya mwombaji wa kwanza.
Katika kuamua maombi haya, sitatilia maanani mambo ambayo wadaawa hawabishanii. Kinachobishaniwa hapa ni kama waleta maombi wamezingatia matakwa ya Kanuni ya 11 (5) (a) ya Kanuni za Mahakama hii katika kuleta maombi haya. Hilo jambo ndilo hasa kitovu cha haya maombi. Kwa hiyo katika kuamua maombi haya nitataka kujiridhisha kama matakwa ya Kanuni ya 11 (5) (a) ya Kanuni za Mahakama hii, yalizingatiwa na katika kufanya hivyo nitarejea kwenye aya ya 8 ya kiapo cha Bwana Mussa ambayo alikuwa akiirejea na kuisisitiza mara kwa mara. Naona nianze na sheria, yaani kanuni husika. Kanuni ya 11 (5) (a) ya Kanuni za Mahakama hii inaeleza kwamba: "(5) Hakuna amri ya kusitisha utekelezaji itakayotolewa chini ya kanuni hii isipokuwa pale Mahakama itakapojiridhisha kwamba— (a) hasara kubwa inaweza kuupata upande unaoomba kusitishwa kwa utekelezaji, iwapo amri hiyo haitatoiewa;" [tafsiri ni ya kwangu] Kwa upande wa kiapo, ili kuonyesha kwamba waombaji watapata hasara na madhara makubwa, Bwana Mussa alinirejesha kwenye aya ya 8 ya kiapo chake kutetea maombi haya. Aya hiyo inaeleza hivi: 6
"8. Kwamba iwapo amri ya kusitisha utekelezaji haitatoiewa, waombaji watapata hasara isiyorekebishika zaidi kufiko mjibu maombi wa kwanza, kwa kuwa kwa sasa waombaji ndio wanaosimamia vizuri mali za mwombaji wa kwanza tofauti na mjibu maombi wa kwanza ambaye muda wake wa uongozi uliisha tarehe 22 Februari 2019 na ambaye aiishindwa kuwasi/isha hesabu sahihi za mwombaji wa kwanza tangu aiipochaguiiwa tarehe 23 Februari 2014, na haii hiyo itasababisha hasara kubwa kwa mali za mwombaji wa kwanza kwa kuangukia mikononi mwa mjibu maombi wa kwanza ambaye si mdhamini waia kiongozi wa mwombaji wa kwanza." [tafsiri ni ya kwangu] Hoja ya wazi ninayotaka kuanzia nayo ni hii; maombi haya yana waleta maombi kumi, ila hakuna jambo lolote katika kiapo cha Bwana Mussa, wala katika hoja zake za mdomo wakati wa usikilizwaji wa maombi haya, linaloonssha kwamba upandG wa mwombaji wa pili hadi mwombaji wa kumi anaweza kupata hasara au madhara yoyote makubwa kutokana na kutokukubaliwa kwa maombi haya. Kwa muktadha huo, maombi haya kwa kadiri yanavyowahusu waombaji wa pili hadi wa kumi hayana msingi, kwa hiyo nayakataa.
Kuhusu mwombaji wa kwanza, nimezingatia kwa makini sana kiini cha aya ya 8 ya kiapo cha Bwana Mussa, na niseme mapema kabisa kwamba ninatofautiana naye kuhusu hoja kwamba eti aya hiyo inaeleza kwa ufasaha kwamba mleta maombi wa kwanza atapata hasara au madhara makubwa endapo maombi haya yatakataliwa. Na nitaeleza kwa ufupi, ni kwa nini nina mtazamo huo. Hoja ya kwanza iliyotolewa na Bwana Mussa kwamba waombaji wanaendelea kusimamia vizuri mali za mleta maombi wa kwanza, ni hoja nyepesi. Hii ni kwa sababu umahiri wa waleta maombi katika usimamizi wa mali za mleta maombi wa kwanza, haithibitishi hasara kubwa kwa upande wao, kwa muktadha wa Kanuni ya 11 (5) (1) (a) ya Kanuni za Mahakama hii. Hoja ya pili ya Bwana Mussa aliyoitoa, ilikuwa ni ya kutoka kwake, yeye kama yeye na si hoja iliyojengwa kwenye msingi wowote kutoka kwenye kumbukumbu zozote ndani ya jalada lililokuwa mbele yangu. Hii ni kwa sababu; kwanza, hapakuwa na jam bo lolote katika kiapo chake lililodhihirisha kwamba palikuwepo na hasara yoyote iliyosababishwa na mjibu maombi wa kwanza kwa mwombaji wa kwanza katika kipindi chake cha miaka mitano kilichotajwa. Pili, Bwana Mussa aliyethibitisha kiapo hicho hakufichua chanzo cha taarifa alizoziapa katika aya hiyo ya 8 ya kiapo chake, kwamba kulikuwa na kutokuwajibika kwa mjibu maombi wa 8
kwanza wakati wa uongozi wake. Aidha, wakili huyo hakuwasilisha nyaraka yoyote kuonyesha kwamba kuiiwahi kuwa na malalamiko kuwa mjibu maombi wa kwanza aliishawahi kusimamia vibaya mali zozote za mwombaji wa kwanza au kwamba alishindwa kutoa taarifa yoyote ya fedha, na hivyo kuna uwezekano mkubwa kwamba jambo hilo linaweza kujirudia akikabidhiwa ofisi. Kwa vyovyote vile, tuhuma za kushindwa kuwasilisha taarifa za kifedha za taasisi kwa wadau, siyo sawa sawa na tuhuma za kuisababishia hasara taasisi husika. Hata na namna au njia za kushughulika na matatizo hayo kisheria hazifanani. Yaani, namna ya kushughulikia mtu aliyeshindwa kutoa taarifa ya fedha, na namna ya kushughulikia mtu aliyesababishia taasisi hasara ni tofauti na matokeo yake hayafanani. Hoja hii inaongezewa nguvu na kushindwa kwa Bwana Mussa katika kiapo chake kuainisha aina au kiwango cha hasara kwa kipindi mjibu maombi wa kwanza alipokuwa ofisini. Katika kesi ya Meis Industries Company Limited v. Exim Bank (Tanzania) Ltd [2017] TZCA 222 Mahakama hii ilisema hivi: "Kuonesha hasara kubwa itakayopatikana ni kipengele cha msingi chini ya Kanuni ya 11 ya Kanuni hizo. Hivyo basi, endapo maeiezo na ufafanuzi wa hasara hiyo hayataainishwa kwa
undani, hakuna msingi wowote ambao Mahakama inaweza kujiridhisha kwamba hasara hiyo itatokea. (Tazama Mechmar Corporation (MALAYSIA) v . Benhard VIP Engineering and Marketing na mwenzake, Maombi ya Madai Na. 184 ya 2008 na Tanzania Cotton Marketing Board v. Cogecot Cotton Co SA [1997] T.L.R. 64." [tafsiri ni ya kwangu] Katika maombi haya, kama ilivyoelezwa wazi wazi hapo juu, hakuna maeiezo yoyote, achilia mbali ya kina, ya hasara inayoweza kutokea endapo, maombi haya yatakataliwa. Kwa hiyo, takwa la kuthibitisha uwezekano wa kutokea hasara au athari kubwa kwa waleta maombi iliyotajwa katika Kanuni ya 11 (5) (a) ya Kanuni za Mahakama hii, halikuthibitishwa. Kabla sijafikia hitimisho la jumla la uamuzi huu, hoja ya Bwana Njoma inataka kujadili uhalali wa maombi ya utekelezaji wa amri ya Mahakama Kuu ambayo hayako mbele yangu. Kwa maana nyingine, hoja hiyo ni suala la kuamuliwa na Mahakama inayoshughulikia maombi hayo, ambayo kwa vyovyote vile, siyo hii. Mwisho kabisa na kwa muhtasari, maombi haya hayakidhi masharti ya Kanuni ya 11 (3) na (5) (a) ya Kanuni za Mahakama hii. Kwa hiyo, 10
nayatupilia mbali na kuelekeza kwamba kila upande utajilipia gharama zake. Imeamriwa hivyo. Hapa DODOMA tarehe 24 Aprili, 2026. Z. N. GALEBA JAJI WA RUFANI Amri imetolewa kwa njia ya mtandao leo tarehe 27 Aprili, 2026 mbele ya Bw. Buruhani Mussa, Wakili wa waombaji, Bw. Juma Nassoro, wakili wa Mjibu maombi wa kwanza, Bw. Swalehe Njoma, Wakili wa Serikali Mwandamizi wa wajibu maombi wa pifi na wa tatu na Bi. Christina Mwanandenje, Karani wa Mahakama; imethibitishwa kama nakala ya ai